|
karibu katika tovuti ya e-agriculture |
|
 Tovuti hii imeanzishwa na Asasi ya Maendeleo ya Vijana [Tanzania Development Forum for Youth] kuwahabarisha wakulima wa Tanzania kuhusu bei za soko za mazao yao mbalimbali ya kilimo wanayozalisha katika misimu yote nchini na pia katika nchi za kusini na mashariki mwa Afrika na soko la dunia. Silaha muhimu sana kwa mkulima wa kitanzania kujiondoa katika ulanguzi wa mazao ya jasho lake ni kumfahamisha na kumpa habari za bei za mazao yake katika ngazi ya nchi na kimataifa pia. Akipata habari hizi muhimu mkulima atakuwa na nguvu ya kupanga bei za mazao yake kwa kujiamini na kwa uhakika zaidi kwani hatadanganywa na kulanguliwa na wafanya biashara wa kati tena. |
|
Soma zaidi...
|
|